Monday, 30 June 2014

TBS WAWATUNIKIA CHETI CHA UBORA TCRA


        KATIKA kuonyesha ubora kwa Watanzania mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) imetakiwa kuongeza juhudi katika kuboreshaji sekta hiyo,  baada ya kukabidhiwa cheti cha kiwango cha kimataifa na Shirika la Viwango Duniani.

        Cheti  hicho kilikabidhiwa jijini Dar es Salaam leo, mbele ya wafanyakazi wote wa TCRA na Mkaguzi wa kimataifa kutoka Uingereza Andrew Rowe na kumpa Mkurugenzi wa TCRA Prof. John Mkoma.

    Akipokea cheti hicho, Profesa Nkoma, alisema kuwa kutokana na utendaji kazi wa mamlaka hiyo katika kudhibiti mawasiliano nchini, ndio sababu iliyopelekea kupata cheti hicho kinachoipa heshima Tanzania.

       Profesa Nkoma, alieleza kuwa umefikia wakati muhafaka wa sekta hiyo kufanya kazi kwa ufanisi ifikapo 2017 ili Shirika hilo litakapokuja kufanya ukaguzi wakute utendaji kazi upo juu.

       “Cheti tulichopata ni ISO 900:2008  kimetokana na ushirikiano tulioana miongoni mwa wafanyakazi wote na sio mkurugenzi peke yake, tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutetea cheti hichi ambacho kinadumu hadi mwaka 2017,” alisema Prof. Mkoma.

    Aidha mkaguzi huyo Andrew Rowe, ilihitaka TCRA kuhakikisha wanapigania katika utoaji wa huduma bora ili kuendelea kubaki na cheti hicho kinachowatambulisha kimataifa.

      “Inatakiwa kuongeza juhudi katika utoaji wa huduma ya mawasiliano kwani ni sekta muhimu kwa taifa hasa Tanzania” alitoa rai Andrew.

       Akizungumzia ubora wa cheti hicho, Mhandisi  kutoka Shirika la Viwango Tanzania  (TBS), Salvatory Rusimbi, alisema kutokana na viwango bora vya kazi, uongozi bora na matumizi bora ya rasilimali zinazo tumika kunufaisha utendaji kazi ndio vitu vilivyochangia kupata cheti hicho.


     “Naipongeza TCRA kwani mkaguzi ameona kazi inayofanywa katika utoaji wa mawasiliano nchini pia utendaji huu utawanufaisha wateja hivyo inatakiwa kuongeza ushirikiano katika kazi” alisema Rusimbi.

Wednesday, 25 June 2014

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAANZA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KWA MFUMO MPYA WA BVR


 “Ili kuwezesha kuwa karibu zaidi na wanancahi na hivyo kupunguza malalamiko ya auambali wa vituo vya kujiandikisha na kuaongeza mwamko wa kujiandikishwa na kupiga kura.” Alifafanua Jaji Lubuva. 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Joseph Mchina, alisema maandalizi yote muhimu kwa ajili ya zoezi hilo katika Manispaa yake yamekamilika na hivyo kuwa na vituo 154 badala ya 84 vya awali.

MAKAMU WA RAIS WA CHINA ATEMBELEA SHIRIKA LA RELI LA TANANIA NA AMBIA TAZARA

MGOMBEA URAIS WA KLABU YA SIMBA BW. EVANS AVEVA AZINDUA KAMPENI ZAKE LEO

1 - CopyMgombea urais wa Kalabu ya Simba ya jijini Dar es salaam Bw. Evans Aveva akizunngmza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Raha Tower jijini Dar es salaam leo wakati akitangaza rasmi uzinduzi wa kampeni zake, uchaguzi wa klabu hiyo unatarajiwa kufanyika Juni 29 kwenye ukumbi wa Police wa Oysterbay jijini Dar es salaam, Kushoto ni Mwenyekiti Mstaafu wa klabu hiyo Mzee Hassan Dalali ambaye ni Meneja wake wa kampeni. 3 - CopyMgombea wa Umakamu wa rais wa klabu hiyo Bw. Godfrey Nyange :Kaburu” akiwa katika mkutano huo uliofanyika katika jengo la Raha Tower jijini Dar es salaam. 4 - CopyKushoto ni Mtangazaji wa Radio One Bw. Maulid Kitenge na Mulamu Ghambi mmoja wa wanachama wa kundi la Friendes Of Simba na mwanachama wa Klabu hiyo wakiwa katika mkutano huo. 5 - Copy Mgombea wa Umakamu wa rais wa klabu hiyo Bw. Godfrey Nyange :Kaburu” naye akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano huo.

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WA CHINA HAPA NCHINI

China 1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Ghalib Bilal kulia akifuatilia burudani zilizokuwa zikitolewa wakati wa Uzinduzi wa Kongamano la Confucius Barani Afrika jana jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao. China 2Wanafunzi wa shule ya Msingi Mlimani ya jijini Dar es Salaam wakitoa burudani katika uzinnduzi huo kwa kuimba nyimbokwa lugha ya kichina. China 3Baadhi ya wageni wakifuatilia kwa makini burudani mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa Uzinduzi wa Kongamano la Confucius Barani Afrika jana jijini Dar es Salaam china 4 Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao akioneshwa machapisho mbalimbali yanayohusu Utamaduni wa watu wa China. China 5Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Ghalib Bilal wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa Uzinduzi wa Kongamano la Confucius Barani Afrika jana jijini Dar es Salaam. FMama Nye 1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao akisalimiana na Mke wa Baba wa Taifa mama Maria Nyerere wakati alipomtembelea nyumbani kwake jana ikiwa ni sehemu ya ziara yake nchini Tanzania. Mama Nye 2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao akimkabidhi zawadi Mama Maria Nyerere jana wakati alipomtembelea nyumbani kwake Msasani.
Mama Nyerere.
Mama Nye 3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafamilia ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere.
Ubalozi 1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Ghalib Bilal kushoto na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao wakimwaga mchanga kwenye jiwe la msingi mahali ambapo ubalozi wa China unatarajiwa kujengwa. Ubalozi 2 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Ghalib Bilal na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yuanchao wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakandarasi wa mradi huo wa ujenzi wa Ubalozi wa China nchini Tanzania. Ubalozi 3Burudani zikiendelea wakati wa kuweka jiwe la msingi mahali ambapo ubalozi wa China unatarajiwa kujengwa mapema jana jijini Dar es Salaam.

Picha zote na Eliphace Marwa – MAELEZO

HABARI MBALIMBALI ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF


tff_LOGO1                                        

SMALL BOYS, MSHIKAMANO, PACHOTO ZAPIGWA FAINI RCL

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zimezipiga faini ya kati ya sh. 300,000 na sh. 500,000 klabu za Mshikamano FC, Pachoto Shooting Stars, Town Small Boys na Kiluvya United kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo viongozi, wachezaji na washabiki kufanya vurugu kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) iliyomalizika hivi karibuni.

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Mashindano ya TFF iliyokutana juzi (Juni 23 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kupitia masuala mbalimbali ikiwemo taarifa za mechi, na malalamiko kutoka kwa baadhi ya timu zilizoshiriki RCL iliyochezwa katika vituo vya Mbeya, Morogoro na Shinyanga.

Town Small Boys ya Ruvuma imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa mujibu wa kanuni ya 37(13) ya Kanuni ya RCL kutokana na udanganyifu kwa kumtumia mchezaji Agaton Mapunda ambaye hakustahili ingawa usajili wake ulithibitishwa na TFF, kwa kutokuwepo pingamizi kutoka klabu yoyote katika kipindi cha pingamizi.

Licha ya usajili wake kuthibitishwa na TFF, Kamati ilibaini mchezaji huyo hakutoka ndani ya Mkoa wa Ruvuma kama kanuni za RCL zinavyoelekeza. Hata hivyo, matokeo ya mechi hiyo dhidi ya Njombe Mji iliyomalizika kwa bao 1-1 yanabaki kama yalivyo kwa mujibu wa kanuni ya Kanuni ya 52 (3 na 4) na 31(11) ya RCL kwa kuwa mchezaji Mapunda alithibitishwa na TFF (qualified player).

Vilevile mchezaji huyo amepigwa faini ya sh. 200,000 kwa mujibu wa kanuni za 48(4) na 31(11) za RCL. Nayo malalamiko ya Njombe Mji dhidi ya mchezaji David Noel Makakala kuwa ndiye aliyecheza mechi hiyo badala ya Carlos Mapunda yametupwa kwa kukosa vielelezo na ushahidi wa kuthibitisha hilo.

Kiluvya United FC ya Pwani imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa mujibu wa kanuni ya 37(1) kutokana na vurugu za washabiki wake kwenye mechi namba 46 dhidi ya Abajalo iliyochezwa mjini Morogoro.

Pachoto Shooting Stars ya Mtwara na Mshikamano FC ya Dar es Salaam zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa kufanya vurugu kubwa kwenye mechi yao namba 100 iliyovunjika mjini Morogoro. Pia Mshikamano FC wamepewa pointi tatu na mabao matatu kwa mujibu wa kanuni ya 23(1na5) na 22(d).
Wachezaji na viongozi wa Pachoto Shooting na wachezaji wa Mshikamano FC waliofanya vurugu na kupigana, suala lao linapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa uamuzi na hatua za kinidhamu.

Nayo Tanzanite ya Manyara imefungiwa kucheza mashindano yote rasmi kwa msimu mmoja, na kuteremishwa daraja hadi ligi ya wilaya mara itakapomaliza kifungo chake kwa mujibu wa kanuni ya 21(3)(a), 37(14) na 22(a). Tanzanite iliadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 23(1,5 na 6) baada ya kumpiga mwamuzi kwenye mechi dhidi ya AFC na baadaye kugomea mchezo. Ilishindwa kulipa faini na kujitoa mashindanoni kwa kuondoka kituoni.

Wachezaji wanaotuhumiwa kumpiga mwamuzi mpaka kumjeruhi suala lao litapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF.

Kamati imetupa malalamiko ya African Sports ya Tanga dhidi ya Abajalo ya Dar es Salaam, Ujenzi FC ya Rukwa dhidi ya AFC, Panone FC ya Kilimanjaro dhidi ya Volcano FC ya Morogoro, na Mvuvumwa FC ya Kigoma dhidi ya Mbao FC ya Mwanza kwa kukosa vielelezo na ushahidi.

Pia malalamiko ya Mvuvumwa FC dhidi ya Geita Veterans ya Geita juu ya kuwachezesha Ibrahim Alphonce, Zamoyoni Magoma na John Mtobesya kwa kuwa hawakusajiliwa yametupwa kwa vile wachezaji hao ni halali, isipokuwa orodha ya wachezaji wa Geita Veterans FC iliyotolewa kwa ajili ya pingamizi ilikuwa na upungufu kiuchapaji ambapo wachezaji sita hawakuorodheshwa
Nao makamishna Edward Hiza na Jimmy Lengwe waliokuwa kituo cha Morogoro wamepewa onyo kutokana na ripoti zao kuwa na upungufu.
  vilevile Kamati ya Mashindano imezitangaza rasmi timu za African Sports, Geita Veterans na Panone FC kupanda kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015

YANGA YAMPATA MARCIO MAXIMO

index
KOCHA Mkuu wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbrazil,  Marcio Maximo anatarajia kuwasili nchini leo mchana akitokea kwao kwa ajili ya kuinoa timu ya soka ya Yanga iliyoanza mazoezi jana.
 
kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Manyara Sports Management, Ally Mleh Maximo anawasili sambamba na msaidizi wake Leonardo Neiva.
Ni kweli kocha Marcio Maximo amekubali kuingia mkataba na timu ya

Yanga ambapo anatarajiwa kuanza kazi rasmi tarehe 27/06/2014 ambapo
atafuatana na msaidizi wake Leonardo Neiva. Mazungumzo ya makubaliano
hayo yalichukua muda mrefu kidogo hatimaye tumefikia
makubaliano.Tunashukuru mungu kila kitu kimekamilika,” alisema Mleh.
 
Mleh alisema Manyara sports Management ni kampuni inayojishughulisha na uwakala wa
wachezaji na makocha, kutafuta wadhamini katika michezo, na usambazaji
wa vifaa vya michezo.
Alisema kwa niaba ya Marcio Maximo anapenda kuushukuru uongozi wa klabu ya
Yanga, kwa kweli wameonyesha  umakini na professional kwa muda wote wa
majadiliano. Nawaomba wachezaji,wanachama na wapenzi wote wa Yanga
wampe ushirikiano.
Baada ya kumaliza mkataba wake wa kuifundisha Taifa Stars nchini
aliingia mkataba na timu kubwa nchini Brazil  mpaka mkataba wake
ulipoisha.Kwa wakati huu kulikuwa na mazungumzo na timu mbalimbali
Zilizotoa  ofa nchini China, Ethiopia na Afrika kusini lakini Yanga
wamefanikiwa kumnasa kocha huyo.

YALIYOTOKEA BUNGENI LEO HII HAPA


PG4A3768 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na  Mbunge wa Mtwara Mjini  Hasnan Murji,bungeni mjini Dodoma Juni 25, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MASHINDANO YA VIJANA AFRIKA MASHARIKI YAANZA

DSC03093
 
Mahmoud Ahmad Arusha
 
Mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 16 kwa nchi za Afrika mashariki yameanza kuchezwa leo jijini Arusha na kuzishuhudia timu kutoka nchi hizo zikianza vyema katika kutafuta kinyang’anyiro cha kutetea ubingwa ambao unashirikiliwa natimu  ya Gaspo Youth kutoka Kenya.
 
Katika mechi 16  zilizochezwa leo  timu ya Chrisc kutoka kenya  na timu ya Buguruni youth kutoka Dar es salaam ziliweza kutoshana nguvu kwa kufungana goli moja kwa moja ,huku Chrisc  2 kutoka kenya imeweza kuibuka na ushindi wa bao 2 dhidi ya wenzao Chrisc ya Tanzania waliopata bao 1,kwa upande ya mechi nyingine Timu ya Msimamo youth imeifunga Buguruni Youth kwa bao 1-0.
 
Mechi ziliendele a ambapo Aspire mega sports academy na Victoria  sports association  zote kutoka kenya  zilitoka nguvu sawa ya bila kufungana,huku mikadini Youth Centre imeichapa bila huruma timu ya Chrisc 2 Kenya kwa magoli 4-1,mechi iliyofuata Buguruni Youth A  ilichapwa bao 1-0 na timu ya Meru Warrious.

 

Mashindano hayo yataendelea tena kesho kwa mechi kuchezwa kwa hatua ya mzungo ambapo jumla ya michezo 26 inatarajiwa kupigwa katika viwanja tofauti
 
Nchi shiriki za mashindano hayo ya mpira wa miguu na mpira wa wavu ni pamoja na Tanzania, Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi,Sudani Kusini,Zambia ,Zanzibar pamoja na Zimbabwe huku wadhamini wa mashindano hayo ni  taasisi ya Chrisc kutoka nchini Norway.

UNAKIFAHAMU KITENDAWILI KATI YA MBASHA NA MKEWE ..................SOMA HAPA...........


Kuna kila dalili kwamba mwimbaji maarufu wa muziki wa Injili nchini,Flora Mbasha na mumewe Emmanuel Mbasha wanatamani kurudiana, baada ya
kuwapo mgogoro katika uhusiano wao wa ndoa, ulioingia katika vyombo vya habari yapata mwezi mmoja sasa.
 
Kwa nyakati tofauti jana, kila mmoja wao alimwambia mwandishi wetu kwamba yupo tayari kurudiana na mwenzake, hatua ambayo inaweza kuondoa mgogoro huo ambao umefifisha taswira yao ya kiutumishi.
 

Akizungumza nyumbani kwake Tabata Kimanga, Dar es Salaam, Mbasha alisema ameshamsamehe mkewe na kwamba anamsubiri muda wowote arudi nyumbani kusuluhisha mgogoro wao.

“Nawapenda Watanzania wote wazidi kutuombea ili mimi na mke wangu
turudiane.”

Kauli hiyo ni sawa na ile aliyoitoa Flora wiki iliyopita pale aliposema: “Ninawaomba Watanzania waendelee kuniombea ili niweze kushinda majaribu haya, kilichotokea ni sehemu tu ya kupimwa imani yangu”.

Tuesday, 24 June 2014

SERIKALI YA UJERUMANI AYAHIDI KUTOA MSAADA WA EURO MILIONI MOJA PORI LA AKIBA LA SELOUS


220px-Coat_of_arms_of_Tanzania.svgSerikali ya Ujerumani, pamoja na ahadi ya Euro milioni moja ya kusaidia Uhifadhi wa Pori la Akiba Selous, imehimiza mataifa mengine kusaidia Uhifadhi wa Pori hilo kutokana na ujangili wa tembo uliokithiri.
Pori la Akiba Selous, lenye ukubwa wa kilometa za mraba 50,000, ni mojawapo kati ya maeneo saba yaliyo kwenye orodha ya Urithi wa Dunia nchini Tanzania. Maeneo mengine  ni Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa Serengeti, Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Magofu ya Kilwa Kisiwani na Magofu ya Songo Mnara, Michoro ya Miambani Kondoa, na Mji Mkongwe Zanzibar. Malengo makuu na faida ya kuweka eneo kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia ni pamoja na:
•    Kuwa na nguvu ya pamoja kimataifa ya kusimamia uhifadhi wa eneo;
•    Kujulikana kimataifa kama kivutio chenye sifa maalum cha utalii;
•    Kutumika kwa tafiti mbali mbali za uhifadhi pamoja; na
•    Kuvutia misaada ya kimataifa ya kiuhifadhi.  
Kamati ya Urithi wa Dunia imeainisha vigezo 10 vinavyowezesha eneo kuorodheshwa kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia.Pori la Akiba Selous liliorodheshwa mwaka 1982 kwa kukidhi vigezo viwili kati ya hivyo, ambavyo ni:
•    Eneo muhimu sana kwa bioanuai ikiwemo idadi kubwa ya tembo kuliko pori lolote duniani; na
•    Eneo lenye aina na muingiliano mpana wa uoto wa asili ikiwemo mimea zaidi ya aina 2100 na  misitu mikubwa aina ya miombo kuliko sehemu nyingine yoyote duniani.
Katika  Mkutano wa 38 wa Kamati ya Urithi wa Dunia unaoendelea jijini Doha-Qatar (15-26 Juni 2014), Pori la Akiba Selous ni mojawapo ya maeneo yaliyoingizwa kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia ulio hatarini.
Lengo la kuingiza eneo kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia ulio hatarini ni kuongeza uelewa wa jamii kitaifa na kimataifa kuhusu matatizo yanayolikabili eneo hilo ili kuwezesha upatikanaji wa misaada ya hali na mali ilikulirejesha katika hadhi yake ya asili.
Tangu Pori la Akiba Selous liwekwa kwenye orodha ya maeneo ya Urithi wa Dunia, hali yake kwa ujumla iliendelea kuwa nzuri na ya kuridhisha. Hata hivyo, kuanzia mwaka 2010 Pori hili pamoja na maeneo mengine nchini yamekumbwa na wimbi kubwa la ujangili, hususani wa tembo. Hali hii imesababisha kupungua kwa idadi ya tembo katika mfumo ikolojia wa Selous, kutoka tembo 70,000 mwaka 2006 hadi kufikia tembo 13,084 mwaka 2013. Kutokana na hali hiyo, Serikali ya Tanzania ilichukua hatua za haraka kudhibiti hali hii katika Pori la Akiba Selous kwa :
•    Kuliongezea uwezo wa rasilimali fedha kwa kurejesha utaratibu wa awali wa kubakiza asilimia 50 ya mapato;
•    Kuandaa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa kuhifadhi tembo na kuunda vikosi maalum vya pamoja miongoni mwa taasisi za wanyamapori vya kupambana na ujangili katika kanda 11 nchini. Mojawapo ya kanda hizo ni kwa ajili ya mfumo wa ikolojia ya Selous;
•    Kuboresha shughuli za uhifadhi rasilimali ya wanyamapori kwa kubadili mfumo wa usimamizi wa uhifadhi wa wanyamapori kwa kuanzisha Mamlaka ya Wanyamapori itakayowezesha Pori la Akiba la Selous kupata fedha za kutosha kwa ajili ya shughuli za uhifadhi;
•    Kuongeza idadi ya wahifadhi wanyamapori 105 ambao 40 kati yao walipangiwa eneo la kazi la Pori la Akiba Selous. Aidha, usaili wa kuajiri wahifadhi wengine 437 umefanyika na kati yao 200 watapangiwa kazi katika Pori la Akiba la Selous; na
•    Kuongeza idadi ya vitendea kazi yakiwemo magari mapya 8, helikopta moja, ukarabati wa mitambo na magari, kuboresha huduma za jamii kwa watumishi pamoja na kukarabati miundo mbinu ya barabara, nyumba za watumishi na viwanja vya ndege.
Kutokana na hali ya ujangili mkubwa uliosababisha kupungua kwa kasi kwa idadi ya tembo,Kamati ya Urithi wa Dunia ilituma timu ya wataalam mwezi Desemba 2013 kwa ajili ya kufanya tathmini ya ukubwa wa tatizo na kupendekeza hatua stahili za kuchukua kunusuru hali hii. Baada ya kutembelea Pori la Akiba Selous na kupata maoni ya Serikali na wadau mbalimbali wa uhifadhi, Kamati ya Urithi wa Dunia ilipendekeza Pori la Akiba Selous liwekwe kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyo hatarini kama ilivyokuwa kwa eneo la Magofu ya Kilwa Kisiwani na Magofu ya Songo Mnara mwaka 2004. Pendekezo hili limeridhiwa na Mkutano wa 38 wa Kamati ya Urithi wa Dunia unaoendelea Doha katika Falme ya Qatar.
Katika mkutano huu,eneo la Magofu ya Kilwa Kisiwani na Magofu ya Songo Mnara limeondolewa kutoka orodha ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyo hatarini baada ya juhudi kubwa za Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na jamii ya kimataifa kuchukua hatua stahili kurekebisha upungufu uliosababisha eneo hili kuwekwa kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyo hatarini. Pori la Akiba Selous kuwekwa katika orodha ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyo hatarini ni fursa ya kuweza kupata misaada kutoka jamii ya kimataifa kwa ajili ya kukabili tatizo la ujangili wa tembo.
Kwa mujibu wa uamuzi huo, Kamati ya Urithi wa Dunia imetoa muda wa mwaka mmoja kwa Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kukomesha ujangili wa tembo katika Pori la Akiba la Selous na hatimaye kuliondoa kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyo hatarini.Kutokana na uamuzi huu, Serikali ya Ujerumani imeahidi kutoa euro milioni moja na kuhimiza mataifa mengine yatoe misaada ya kifedha na kiufundi kwa Tanzania ili iweze kukabili tatizo hili sugu haraka iwezekanavyo.  Vile vile mataifa mengine ikiwemo Ureno, Algeria, Senegali, Lebanon na Colombia yameungana na Ujerumani kuhamasisha jumuiya ya kimataifa kuisaidia Tanzania kutimiza azma yake.
IMETOLEWA NA MSEMAJI WA WIZARA
23.06.201

CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO SUA CHATILIANA SAINI YA MAKUBALIANO YA KUTUMIA MATOKEO YA UTAFITI KUDHIBITI UGONJWA WA NDUI YA KUKU NA KAPUNI YA MCI SANTE ANIMALE.DAR ES SALAAM




HABARI GANI WATU WANGU WASOMAJI WA BLOG YA YALIYOMO YAMO BLOG
DAAAH NKO ,MKOANI WATU WANGU WA NGUVU NI PANDE ZA CHUGA IVI APA FULL BARIDI KWA SAANA NATAMANI NIRUDI MAHOME TOWN DAR /////////////

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00207
MWENDESHA PIKIPIKI MMOJA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE JINSI YA KIUME, MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 25 – 30 AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 23.06.2014 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU KATIKA ENEO LA CHAPWA, KATA YA CHIWEZI, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. MAREHEMU ALIKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.419 BRA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. JITIHADA ZA KULITAFUTA GARI NA DEREVA ZINAFANYWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
TAARIFA ZA MISAKO:
MSAKO WA KWANZA:
MFANYABIASHARA MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JULIUS ERNEST (27) MKAZI WA KANGA, WILAYANI CHUNYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIUZA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA  BOSS PAKETI 15.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 23.06.2014 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA KANGA MADUKANI, KATA YA   KANGA, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA AMEFIKISHWA MAHAKAMANI CC 98/2014 NA KULIPA FAINI TSHS 100,000/= -ERV 50360638.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII NA WAFANYABIASHARA KUACHA KUJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
MSAKO WA PILI:
MFANYABIASHARA MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BWIGANE MKAMBALA (32) RAIA NA MKAZI WA NCHINI MALAWI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA AMEINGIA NCHINI KINYUME CHA SHERIA.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 23.06.2014 MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI KATIKA MAENEO YA BULYAGA, KATA YA BULYAGA, TARAFA YA TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MHAMIAJI HARAMU, TARATIBU ZA KUMKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAFANYWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO ILI UPELELEZI DHIDI YAO UFANYWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

WASHINDI WA TMT KUTOKA KANDA YA ZIWA NA NYANDA ZA JUU KUSINI WAWASILI DAR ES SALAAM TAYARI KWA SAFARI YA KUSHINDANIA MILIONI 50


Washindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kutoka Kanda ya Ziwa wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere, Jijini Dar Es Salaam jana kwaajili ya Kuin
gia kambini tayari kwa safari ya kushindania Milioni 50 katika fainali itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa Nane
 
 Washindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kanda ya Nyanda za Kusini, Stephen Mapunda(mwenye kofia nyekundu) na Mtawa Kaparata (mwenye fimbo) wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere jana tayari kwa safari ya kushindania Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
 Washindi wa Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini wakibadilishana Mawazo wakati walipowasili katika uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere, Jijini Dar Es Salaam jana.
 Washindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) wakielekea kwenye basi la TMT tayari kwa kupelekwa kwenye Hoteli kwaajili ya Kupumzika mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere, Jijini Dar Es Salaam. 


Washindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kutoka kanda zote za Tanzania wamewasili jijini Dar Es Salaam jana kwaajili ya kuingia kambini tayari kwa Kuanza safari ya kushindania kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Shindano la TMT itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa Nane.

Fainali hiyo ya aina yake inayotarajiwa kutoa Mshindi mmoja mkubwa ambae ataondoka na Kitita cha Shilingi Milioni 50 ambapo washindi wengine tisa wakiungana na mshindi mmoja watacheza filamu ya pamoja ambayo itauzwa na kusambazwa na Kampuni ya Proin Promotions na washiriki hao kuweza kunufaika na Mauzo ya filamu hiyo.

Mara baada ya washindi 20 kutoka kanda zote sita wataingia Kambini mara baada ya kutoka kupima afya zao na hatimaye mchakato wa kumpata mshindi mmoja wa Shilingi Milioni 50 kuanza. Katika hatua hii ya kuanza kumtafuta mshindi wa milioni 50, Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) watakuwa wamepunguziwa majukumu kwa asilimia 40 na kazi hiyo kuelekea kwa wananchi ambapo watawapigia kura washiriki ambao wanawaona Wana vipaji na uwezo wa kuigiza.

Zoezi hilo la Upigaji kura litaanza mara moja mara baada ya washindi hao kuingia rasmi kambini na kuanza kupewa shule ya Sanaa na Walimu kutoka Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo.