|
Mgeni rasmi katika siku ya sherehe ya wahitimu wa kiislam akifafanua jambo kwa waumini wa kiislamu wa jumuiya ya wanafunzi wailam wa chuo cha taifa cha usafirishaji. Mgeni huyo amewataka waislam kushikamana na usilamu wao hata huko wanakoenda makazini kwani kufanya hivyo kunampendeza sana mwenyezi mungu kuliko kuuacha uislam wa mtu kisa umefanikiwa kupata elimu. |
|
Baadhi ya wahitimu wa chuo hicho wakifuatilia kwa makini hutuba ya mgeni rasmi juu ya waislamu kushikamana na dini yao, hata hivyo katika sherehe hizo waislamu hao walitoa dukuduku lao juu ya kutaka kujengewa msikiti kitu ambacho mgeni huyo amesema yeye yupo tayari kujitolea mafari yote ambayo yatatakiwa kwa ajiri ya ujenzi. |
|
Ummati wa kiilsamu wakiwa katika sherehe hizo zilizofanyika katika ukumbi wa recreation katika viwanja vya chuo.Mstari wa mbele kabisa ni amiri wa jumuiya ya kiislam MSANIT wakifuatilia kwa makini mwenendo wa hutuba katika siku hiyo. |
|
Mmoja wa viongozi shupavu katika chuo hicho akipokea cheti chake toka jumuiya ya Kiislam Msanit wakati wa mahafari hayo |
Jumuiya ya kiislam, katika chuo cha taifa cha usafirishaji NIT (MSANIT) wametoa wito kwa muislam yeyote na hata yule ambae hajabahatika kuwa muislam kujitolea kwa moyo wa dhati ili ujenzi wa mskiti katika chuo hicho uchukue hatua zake,
Wakizungumza na mtandao huu hivi karibuni katika mafahari ya jumuiya hiyo, mmoja wa maamiri mkubwa kabisa wa ngazi ya juu ambaye amesita kutoa jina lake hadharani, amesema kwa sasa jumuiya yake inatatizo kubwa la kifedha ili kujenga msikiti ambao kwa muda mrefu ramani yake tayari imeshakamilika
Amiri amesema, hatua zote za awali tayari zimeshakamilika na kwamba kitu kikubwa ambacho kwa sasa kinasumbua ni upatikanaji wa fedha za kuanza ujenzi mara moja,
No comments:
Post a Comment