UNICEF Tanzania yawateua AY na Faraja K. Nyalandu kama Mabalozi wao wakuhamasisha umma juu ya ukatili dhidi ya watoto
Katika kusherehekea siku ya Mtoto
wa Afrika tarehe 16 Juni, Halmashauri ya Wilaya ya Hai, ikishirikiana na
viongozi wa serikali, UNICEF na Save the Children, imezindua Kituo cha
Huduma Jumuishi, kitakachowasaidia wanawake na watoto ambao wameathiriwa
na ukatili.
“Katika kituo hiki, huduma za
kuwasaidia wahanga wa ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto
ikiwa ni pamoja na huduma za afya, msaada wa kisaikolojia,
ulinzi/usalama na msaada wa kisheria vinaweza kutolewa hapo katika eneo
moja ndani ya kituo cha afya zikiwa zimeratibiwa vizuri Zaidi,” alisema
Charles Pallangyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Aliongeza, “kituo hiki kitasaidia
kupunguza madhara zaidi ya ukatili kwa sababu wahanga wa ukatili
wataweza kupata huduma zote muhimu katika eneo moja na hawatakuwa na
sababu ya kurudiarudia kuwaeleza watoa huduma mbalimbali walio katika
maeneo tofauti yale mambo mabaya waliyoyapitia, au kutakiwa kwenda na
kurudi kutokana na ukosefu wa uratibu na uwezo wa watendaji wa sekta
mbalimbali katika kuwahudumia wahanga wa ukatili kwa ukamilifu.”
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dk.
Jama Gulaid, anaamini kuwa kama tukifanya kazi kwa ushirikiano na
serikali na wadau wengine, tunaweza kupata suluhu katika kumaliza
ukatili dhidi ya watoto. “Ukatili dhidi ya watoto uko kila mahali na
hatuwezi kuendelea kuufumbia macho. Watoto wote hapa Tanzania wanahaki
ya kuishi na kukua katika mazingira yasiyo na ukatili. Kama sisi sote
tukifanya kazi kwa kushirikiana pamoja, sina shaka tutaweza kumaliza
ukatili dhidi ya watoto.”
Katika tukio hili huko Hai, UNICEF
Tanzania imemteua msanmahiri wa bongo flava Ambwene Yessyah,
anayejulikanakamaAY, pamoja na aliyewahi kuwa Miss Tanzania,
FarajaKotta Nyalandu kama Mabalozi wao katika ‘Kampeni ya Tokomeza
Ukatili Dhidi ya Watoto.’ Wote wameahidi kusaidia kampeni ya ‘Kampeni ya
Tokomeza Ukatili Dhidi ya Watoto’ na wameonyesha kuhamasishwa na
heshima hii waliyopewa kutoa sauti zao kutetea ulinzi wa mtoto.
Kumekuwa na maendeleo katika
kuboresha hali hii. UNICEF inasaidia serikali ya Tanzania kupitia Idara
ya Ustawi wa Jamii kuanzisha na kuboresha ‘mifumo ya Ulinzi wa Mtoto’
katika halmashauri 13. Katika halmashauri hizi, afya, ustawi wa jamii,
polisi, sekta za elimu na mahakama, magereza, wanasheria,asasi za
kiraia pamoja na mifumo ya kijamii isiyo rasmi wanaunda
Timu ya
Halmashauri ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto na wanashirikiana kuhakikisha
kuwa kesi za ukatili wa watoto zinashughulikiwa vyema na pia wanazuia
ukatili kwa kuongeza uelewa wa jamii juu ya ukatili dhidi ya watoto.
Lengo la Idara ya Ustawi wa Jamii ni kupanua utaratibu wa mfumo huu
katika halmashauri 30 ifikapo mwaka 2016.
No comments:
Post a Comment