Sunday, 15 June 2014

MALINZI ASIMAMISHA UCHAGUZI SIMBA, KISA KAMATI YA MAADILI

MalinziNa Baraka Mpenja, Dar es salaam
RAIS wa shirikisho la soka Tanzania, TFF, Jamal Emil Malinzi, jana aliwaalika waandishi wa habari akiwaomba wafike leo mchana majira ya saa 6:00  katika ofisi za shirikisho hilo kwa lengo la kutoa ujumbe kwa umma wa wapenda michezo Tanzania.
Wengi hawakupata majibu juu ya nini Rais Malinzi anataka kuzungumza na wanahabari kwasababu si kawaida yake kufanya mikutano na waandishi mara kwa mara.
Akitokea Brazil kwenye mkutano wa 64 wa FIFA hivi karibuni, hatimaye mchana wa leo, Rais Malinzi amekutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa shirikisho hilo, uliopo makao makuu katikakati ya jiji la Dar es salaam na kutangaza kusimamisha mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Simba ulioatarajia kufanyika juni 29 mwaka huu hadi hapo itakapounda kamati ya Maadili itakayokuwa na jukumu la kusikiliza masuala ya maadili kuelekeza uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment