Mahmoud Ahmad Arusha
Mashindano ya vijana chini ya
umri wa miaka 16 kwa nchi za Afrika mashariki yameanza kuchezwa leo
jijini Arusha na kuzishuhudia timu kutoka nchi hizo zikianza vyema
katika kutafuta kinyang’anyiro cha kutetea ubingwa ambao unashirikiliwa
natimu ya Gaspo Youth kutoka Kenya.
Katika mechi 16 zilizochezwa
leo timu ya Chrisc kutoka kenya na timu ya Buguruni youth kutoka Dar
es salaam ziliweza kutoshana nguvu kwa kufungana goli moja kwa moja
,huku Chrisc 2 kutoka kenya imeweza kuibuka na ushindi wa bao 2 dhidi
ya wenzao Chrisc ya Tanzania waliopata bao 1,kwa upande ya mechi
nyingine Timu ya Msimamo youth imeifunga Buguruni Youth kwa bao 1-0.
Mechi ziliendele a ambapo Aspire
mega sports academy na Victoria sports association zote kutoka kenya
zilitoka nguvu sawa ya bila kufungana,huku mikadini Youth Centre
imeichapa bila huruma timu ya Chrisc 2 Kenya kwa magoli 4-1,mechi
iliyofuata Buguruni Youth A ilichapwa bao 1-0 na timu ya Meru Warrious.
Mashindano hayo yataendelea tena
kesho kwa mechi kuchezwa kwa hatua ya mzungo ambapo jumla ya michezo 26
inatarajiwa kupigwa katika viwanja tofauti
Nchi shiriki za mashindano hayo ya mpira wa miguu na mpira wa wavu ni pamoja na Tanzania, Kenya,Uganda,Rwanda,Burundi,Sudani Kusini,Zambia ,Zanzibar pamoja na Zimbabwe huku wadhamini wa mashindano hayo ni taasisi ya Chrisc kutoka nchini Norway.
No comments:
Post a Comment