Mwenyekiti
wa kamati ya usajili ya Simba sc, keptein wa zamani wa JWTZ, Zacharia
Hans Poppe anasubiri viongozi wapya ili awasainishe mikataba wachezaji
wapya.
Kwa sasahakuna jambo la msingi
kwa klabu ya Simba zaidiya kufanya uchaguzi wa kumpata rais mpya,
makamuwaraisnawajumbe wa kamati ya utendaji ilimasualamengineyaendelee.
Kumekuwepo na mvutano mkubwa
baina ya wanachama juu ya mizengwe inayogubika uchaguzi wa klabu hiyo,
lakini chanzo cha matatizo hayo ni pale jina la Mgombea Urais Michael
Wambura lilipoenguliwa na kamati ya uchaguzi chini ya mwenyekiti wake
Wakili Dkt. Damas Daniel Ndumbaro.
Mwisho wa siku, lazima ifahamike
kuwa kila palipo na wengi pana mengi na wanapokutana watu zaidi ya
wawili, lazima kutofautiana kwa mawazo kutokee. Mivutano kama hii ni
jambo la kawaida katika chaguzi za kidemokrasia kwasababu kila mtu ana
haki ya kumtetea anayemtaka.
Ukiona watu zaidi ya 100
mnakubaliana kirahisi,kunaweza kuwa na mambo mawili, moja: kuna kiongozi
wa mawazo anayetegemewa hivyo wote mnamfuata na pili kuna uoga kwa
baadhi ya watu kusema ya moyoni.
Kuvutana ni jambo zuri kwasababu
mnakosoana na kuwekana sawa ili kufikia lengo moja. Kukosoa mtazamo wa
mtu ni jambo jema wala halina tatizo lolote. Cha msingi hoja ipingwe kwa
hoja. Unayepinga hoja ya mwenzake, alete hoja mbadala na usilete vurugu
na matusi.
No comments:
Post a Comment