Friday, 13 June 2014

KUNA MKONO WA MTU KUCHOMWA KWA SOKO LA MCHIKICHINI........HISTORIA INAONYESHA;;HENRY KILEO


 
SOMA KAULI YA KISHUJAA YA HENRY KILEO HII HAPA.......................................
 
"Nikiwa kama kiongozi wa Chama ndani ya jiji la Dar es salaam, ninalaani tukio la uchomwaji moto la wafanyabiashara wadogo Karume jijini Dar es salaam. Kilichofanyika ni unyama wa hali ya juu na unapaswa kupingwa na wananchi wote.
 
Historia inaonyesha kuwa kila serikali itakapo Wafanyabishara kuondoka maeneo fulani ya biashara basi maeneo hayo hukubwa na moto. Mfano Mwanga kilimanjaro, Moshi, mbeya na sasa Dar es salaam.
 
Ili kukomesha vitendo hivi dhalimu wafanyabiashara wa Karume popote pale mlipo unganisheni nguvu zenu kupinga udhalimu huu na Kamwe msiondoke mpaka mtakapo pata haki zenu za msingi ikiwamo haki ya kulipwa gharama ya hasara mliyoingia..
 
Kumbukeni Haki haiombwi bali huchukliwe(Nobody can give u freedom but you take it )"
 Henry Kilewo

No comments:

Post a Comment