Thursday, 12 June 2014

URAGHBISHI WA TGNP WAONYESHA MAFANIKIO MAKUBWA KWA WALALA HOI


             Kazi iliyofanywa na mtandao wa jinsia Tanzania GTNP umeanza kuonyesha mafanikio yake baada ya utafiti wa kiragabishi katika kata za Kiroka,wilaya ya Morogoro vijijini,Kata ya Mondo wilaya ya Kishapu, Kata ya Tembela mkoani Mbeya, Kata ya Nyamaraga Mkoani Mara na Kata ya Mabibo Wilaya ya Kinondoni kuonyesha wazi dalili za mafanikio katika matatizo yao mbalimbali,

Akizungumza na Mtandao huu, Mkurugenzi Mtendaji Wa Mtandao wa jinsia Tanzania, Bi. Lilian Liundi amesema katika tafiti ambazo Mtandao huo umeziendesha umegundua matatizo mbalimbali, ambapo wananchi katika maeneo hayo wameanza kuamka baada ya kuchokozwa na wawezeshaji toka katika mtandao,

KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA MTANDAO WA KIJINSIA HAPA NCHINI (TGNP) LILLIAN LIUNDI AKIFAFANUA JAMBO KUHUSU MREJESHO WA URAGBISHI ULIOFANYIKA 9-31 MARCH MWAKA HUU. KATIKA URAGBISHI HUO WANANCHI WALIWEZA KUCHOKOZWA NA WAKACHOKOZEKA NAHIVYO KUFANIKIWA KUDAI HAKI ZAO KWA WAKATI.
MWEZESHAJI WA REPOTI INAYOHUSU URAGBISHI ULIOFANYIKA KATIKA VIJIJI VITANO HAPA NCHINI  (MWENYE NGUO NYEKUNDU ALIYESHIKA MAIKI)AKIWASILISHA TAARIFA YAKE KWA WADAU, JUMLA YA MAMBO MBALIMBALI YALIWEZA KUWASILISHWA IKIWEMO FAIDA ZA URAGBISHI ZILIZOPATIKANA KATIKA KATA HIZO TANO
MARJORIE MBILINYI WA TGNP AKIFAFANUA BAADHI YA MAMBO.

No comments:

Post a Comment