Ofisa
habari wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vusso
(kushoto) akionesha taarifa ya Umoja wa Mataifa ya utekelezaji wa mpango
wa pamoja wa mashirika ya Umoja wa mataifa hapa nchini. Taarifa hiyo
imo katika documentary (taarifa ambayo iko katika mfumo wa video) ya
dakika saba inayoonyesha kazi mbalimbali Umoja wa Mataifa nchi
itazinduliwa leo kwenye ukumbi wa Ngome Kongwe kuanzia saa moja jioni
katika mpango wa Umoja wa Mataifa wa kutumia mitandao ya kijamii
kuwafikia wadau wake wa maendeleo.
Mkuu
wa mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Anna Liboro Senga (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo kuhusu uzinduzi
wa mfumo mpya wa utoaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuli za
maendeleo kwa wadau wake.Mpango huo unazinduliwa leo jioni katika ukumbi
wa wazi wa Ngome Kongwe. Kushoto ni Ofisa habari wa Kitengo cha habari
cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vusso .
No comments:
Post a Comment