Monday, 16 June 2014

WATOTO ZAIDI YA 800 WALAWITIWA KWA KIPINDI KIFUPI TU CHA MWAKA JANA, LHRC WATOA TAMKO KALI


Kaimu wa  LHRC Wakili Sungusia akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika huko Kijitonyama ofini kwake


Hali ya kutothaminiwa kwa haki za watoto hapa nchini imeendelea kuwa tatizo baada yawatoto zaidi ya laki nane kuonekana kulawitiwa huku wanaohusika na ushenzi huo wakionekana wanalandalanda bila kuchukuliwa hatua za msingi hoja kubwa ikiwa ni uhusiano wa karibu kati ya mtoto aliyerawitiwa na mlawiti,

 

Akizungumza na waandishi wa habari hapa Ofisini Kwake katika maazimisho ya siku ya mtoto wa afrika hapa nchini , Kaimu mkurugenz wa Kituo Cha sheria na haki za binadam, Wakili Harodia Sungusia amesema haki za mtoto hapa nchini zimekuwa zikidorola kwa asilimia kubwa ingawaje kuna jitihada za kulinda haki za watoto,
 
Sungusia anasema Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa jumla ya watoto 863 wamelawitiwa lakini takwimu hazisemi ni jumla ya waharifu wangapi ambao wamefikisha katika mahakama na hukumu ngapi zimeshapitishwa dhidi ya ushenzi huo unaofanywa na watanzania wachache kwa watoto hao wadogo,
 
“Tayari tunatakwimu hapa juu ya haki za watoto zinavyovunjwa, lakini hatujui ni wangapi wamechukuliwa hatua, tunadhani sasa wizara ya watoto lazima waliangalie hili kwa makini kwani kunyamaza kimya ni sawa na kuvunja haki za watoto ambao ndio taifa la kesho,” Aliongeza Sungusia

Sungusia amebainisha baadhi ya sababu za haki za watoto kuminywa kuwa ni pamoja na walezi, ndugu, na wazazi wao wa damu kutokuwa tayari kuwafichua wanovunja haki za watoto, kwa mfano hawa ambao wanalawitiwa, kama kuna mtu mwenye ujasiri basi haki ya mtoto ingepatikana 
 
“Unakuta mtoto amelawitiwa na baba mdogo au shangazi yake ama baba ya ke mkubwa sasa mzee kulifikisha suala hilo mahakamani anaona ni shida hivyo ananyamaza kimya na maswala hayo yanamaliza kimila na mwishowe haki ya mtoto inapotea kisa tu aliyefanya unyama huo ni ndugu yake wa damu, kwa kweli hili alikubaliki,”Aliongeza Wakili Sungusia
 
Aidha katika hatua nyingine Wakili Sungusia ametaja haki zingine ambazo mtoto wa afrika amekuwa akionewa ni pamoja na watoto kutumikishwa na kufanyishwa kazi hatarishi. Utafiti unaonyesha kuwa mpaka sasa watoto wa Kiafrika bado wanafanyishwa kazi ngumu na hatarishi kama zile za migodini,viwandani na wengine wamelazimishwa kujiunga katika majashi ya waasi kama yale ya Joseph Koney wa Uganda, na M23 ya Congo na vikundi vya kiagaidi vya Alshabaab nchini Somalia
 
Kumekuna na mwendelezo wa watoto kubaguliwa na kunyanyapaliwa, hii ni tatitzo kubwa kwa ustawi wa watoto wetu hasa hapa barani Afriaka, ambapo sasa imekuwa ni kawaida kwa wazzazi na walezi kuwaficha watoto wao kisa ni walemavu wa viungo fulanifulani hatua inayomfanya mtoto aliyefichwa kukosa haki yake ya msingi ya Elimu,Afya,Malezi bora, na LIshe
Kutekwa , kuuzwa na kusafirishwa kimagendo , Afrika bado inachangammoto kubwa ya watoto wake kutekwa  na kupelekwa sehemu mbali ili wakauzwe kwa lengo la kuwatumikisha katika nchi za ng’ambo, hakika hili ni tatizo ambalo linahitaji utatuzi wa haraka kama kweli tunataka kulinda haki za mtoto Wa Afrika.
 
LHRC WATOA WITO KWA VIONGOZI WA DINI, kuanza kulinda haki za watoto kwani watoto ni taifa la kesho,

No comments:

Post a Comment