Thursday, 12 June 2014

POLISI WAKAMATA VIPANDE 54 VYA MENO YA TEMBO

        
      Katika tukio la kwanza, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaa limefanikiwa kuwakamata watu  watatu kwa tuhuma za kupatikana na vipande 26 vya meno ya Tembo kinyume cha sheria.

           Tukio hili lilitokea  tarehe 29.05.2014 huko maeneo ya M’nyamala Kata ya Mwinyijuma Osterbay (M) Kinondoni baada ya  kupata taarifa toka kwa msiri kuwa kuna gari namba  T 178 BSY NOAH inasemekana ina mizigo ya wizi.

         Baada ya taarifa hizo askari walijipanga na kuweka mtego na kufanikiwa kulikamata gari tajwa hapo juu na walipolipekuwa walikuta viroba viwili vilivyokuwa na vipande hivyo vya meno ya tembo ambavyo thamani yake haikufahamika mara moja.

        Watuhumiwa pamoja na gari husika vinashikiliwa.. Watuhumiwa hao ni kama ifuatavyo:
·       ADAM S/O YONA, miaka 37,  mkazi wa Mbagala, 
·       SELEMANI S/O LEONALD, Miaka 37, Mkazi wa M’nyamala,
·       HUSSEIN S/O SAID, Miaka 34,
Katika tukio la pili, mnamo 05/06/2014 Polisi Wilaya ya Buguruni mkoa wa kipolisi Ilala kwa kushirikiana na bwana BAKARI S/O YUSUF, Miaka 33, Mhifadhi Wanyamapori Makao Makuu, Mkazi wa Mbezi Beach, walifanikiwa kukamata vipande 28 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya Tshs 275,550,000/= nyumbani kwa DOMINICK S/O KOLINELI @ KOMBE, Miaka 35, Mkazi wa Tabata Kisukuru.  

       Walipofanya  upekuzi katika nyumba hiyo ambapo kwenye chumba kimoja cha uwani  cha bwana HERBERT S/O REVIL MACHAKA, Miaka 30, mkazi wa Morogoro, ambapo kilipatikana kipande 1 cha jino la Tembo. Upekuzi uliendelea kwenye Stoo na Jiko  na walipata vipande 27 vya meno ya tembo na kufanya jumla ya vipande hivyo kuwa 28. Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kubaini mtandao mzima wa ujangiri huu unaomaliza rasilimali za taifa. 

No comments:

Post a Comment