CORE founder of Puku AKIONYESHA CHAJA MUHIMU KWA SIMU ZA SMART FONES. |
WATUMIAJI wa simu za kisasa za Smart Phone wametakiwa kutumia chaji za Puku kuchajia simu zao ili kujihakikishia usalama wake.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa chaji hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUKU alisema kuwa chaji hizo kwa sasa zinapatikana hapa nchini.
Alisema kuwa ni chaji ambazo zinahifadhi umeme kwa muda mrefu ambao unakuja kutumiwa kuchajia simu hasa pale ambapo panakuwa hakuna umeme.
Aliongeza kuwa bei yake kwa sasa ni kuanzia 160,000 kutokana na ubora wake na pamoja na namna ambavyo inasaidia.
"Mimi ni mtanzania kutoka Tanga na nilisoma hapa hapa ila nilielekea Marekani kusoma na ninaishi huko na nimebuni hii chaji kwa lengo la kusaidia watu mbalimbali ambao wanakuwa wakisumbuliwa na tatizo la kuchajia simu zao pale ambapo panakuwa hakuna umeme wa uhakika"alisema Meck Mbwana ambaye ni mvumbuzi na mkurugenzi mtendaji wa PUKU.
Aliongeza kuwa " kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya simu za smart phone huku watumiaji wakilalama kuwa wanakosa uhakika wa umeme wa kuzihudumia sasa hii bidhaa itasaidia".
No comments:
Post a Comment