Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (kulia)
akiangalia jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Shirika la Reli la Tanzania
na Zambia (TAZARA) mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya shirika hilo
leo jijini Dar es Salaam kwenda kuangalia miundo mbinu ikiwemo mabehewa
na injini za treni za shirika hilo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (kushoto)
akiangalia ramani ambayo reli ya TAZARA inapita kuanzia kituo cha Dar es
Salaam wakati alipotembelea Makao Makuu ya Shirika la Reli la Tanzania
na Zambia (TAZARA) leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia
miundo mbinu ikiwemo mabehewa na injini za treni za shirika hilo. Kulia
ni Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe.
Waziri
wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe akishuka toka ndani ya treni ya
abiria ya TAZARA kuelekea katika kituo cha mizigo cha TAZARA kilichopo
mtaa wa Yombo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment