Monday, 30 June 2014

TBS WAWATUNIKIA CHETI CHA UBORA TCRA


        KATIKA kuonyesha ubora kwa Watanzania mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) imetakiwa kuongeza juhudi katika kuboreshaji sekta hiyo,  baada ya kukabidhiwa cheti cha kiwango cha kimataifa na Shirika la Viwango Duniani.

        Cheti  hicho kilikabidhiwa jijini Dar es Salaam leo, mbele ya wafanyakazi wote wa TCRA na Mkaguzi wa kimataifa kutoka Uingereza Andrew Rowe na kumpa Mkurugenzi wa TCRA Prof. John Mkoma.

    Akipokea cheti hicho, Profesa Nkoma, alisema kuwa kutokana na utendaji kazi wa mamlaka hiyo katika kudhibiti mawasiliano nchini, ndio sababu iliyopelekea kupata cheti hicho kinachoipa heshima Tanzania.

       Profesa Nkoma, alieleza kuwa umefikia wakati muhafaka wa sekta hiyo kufanya kazi kwa ufanisi ifikapo 2017 ili Shirika hilo litakapokuja kufanya ukaguzi wakute utendaji kazi upo juu.

       “Cheti tulichopata ni ISO 900:2008  kimetokana na ushirikiano tulioana miongoni mwa wafanyakazi wote na sio mkurugenzi peke yake, tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutetea cheti hichi ambacho kinadumu hadi mwaka 2017,” alisema Prof. Mkoma.

    Aidha mkaguzi huyo Andrew Rowe, ilihitaka TCRA kuhakikisha wanapigania katika utoaji wa huduma bora ili kuendelea kubaki na cheti hicho kinachowatambulisha kimataifa.

      “Inatakiwa kuongeza juhudi katika utoaji wa huduma ya mawasiliano kwani ni sekta muhimu kwa taifa hasa Tanzania” alitoa rai Andrew.

       Akizungumzia ubora wa cheti hicho, Mhandisi  kutoka Shirika la Viwango Tanzania  (TBS), Salvatory Rusimbi, alisema kutokana na viwango bora vya kazi, uongozi bora na matumizi bora ya rasilimali zinazo tumika kunufaisha utendaji kazi ndio vitu vilivyochangia kupata cheti hicho.


     “Naipongeza TCRA kwani mkaguzi ameona kazi inayofanywa katika utoaji wa mawasiliano nchini pia utendaji huu utawanufaisha wateja hivyo inatakiwa kuongeza ushirikiano katika kazi” alisema Rusimbi.

No comments:

Post a Comment