TAARIFA RASMI YA MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI WA SIMBA SC, WAKILI DKT. DAMAS DANIEL NDUMBARO KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUPINGA MAAMUZI YA RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI KUSIMAMISHA UCHAGUZI WA SIMBA SC
Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club, ilifanya mkutano
wake kawaida tarehe 15 Juni 2014 kujadili mambo mbalimbali ambayo
yanayohusu uchaguzi mkuu wa Simba Sports Club ambao umepangwa kufanyika
tarehe tarehe 29 Juni 2014. Kamati ya Uchaguzi ya Simba sports Club
inapenda kuujulisha umma, hususan wapenzi wa Simba Sports Club mambo
yafuatayo
1. Kamati ya Uchaguzi ya Simba
Sports Club, kwa mujibu wa Ibara ya 10(6) ya Kanuni za uchaguzi za TFF
toleo la mwaka 2013, ndiyo chombo pekee chenye mamlaka ya kutangaza,
kubadilisha, kusimamisha au kufuta tarehe ya Uchaguzi ya Simba Sports
Club. Kwakuwa Kamati haijafanya hivyo, wala hakuna mdau yoyote aliyeleta
hoja ya kusimamisha uchaguzi, tunawajulisha kuwa uchaguzi wa Simba
Sports Club upo pale pale kama ambayo Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports
Club ilivyopanga. Maandalizi ya uchaguzi huo yanaendelea vema na
Uchaguzi utafanyika tarehe 29 Juni 2014 kama ilivyopangwa hapo awali.
2. Kamati imesikia kupitia vyombo vya habari kuwa TFF imesimamisha uchaguzi wa Simba Sports Club mpaka hapo Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club itakapoteua Kamati ya Maadili. Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club
No comments:
Post a Comment