DARASA LAIVA:
Nimewaua!: Mshambuliaji wa Yanga sc, Jerryson Tegete ( wa kwanza kushoto) akishangilia moja ya bao lake msimu uliopita na wachezaji wenzake, Mrisho Ngassa (katikati) na Saimon Msuva (kulia).
MSHAMBULIAJI wa Yanga sc, Jerryson John Tegete amefurahishwa na viwango vya timu zinazoshiriki kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil japokuwa bado michuano ni mibichi kabisa.
Tegete amezungumza na Mtandao huu mchana huu na kueleza kuwa Cameroon ilianza kwa kufungwa na Mexico bao 1-0, lakini walikuwa na nafasi ya kufanya vizuri.
“Timu za Afrika zimejiandaa vizuri. Cameroon wangekuwa makini wangefaya vizuri”. Alisema Tegete.
“Nimewaona Ivory costa wakicheza, sio wabaya, kuna makosa machache wanafanya na wanapoteza nafasi nyingi, lakini nadhani wawakilishi wa Afrika watafanya vizuri tu”.
Tegete aliongeza kuwa kitu alichojifunza kwa mechi hizi za mwanzo ni timu kucheza kitimu zaidi na si mchezaji mmoja mmoja, jambo ambalo amelipenda na angetamani wachezaji wenzake wajifunze.
No comments:
Post a Comment